TANGAZO LA KAZI JESHI LA ZIMA MOTO NA UOKOAJI

Position: Sajini Wa Zimamoto na Uokoaji (Sergeant of Fire and Rescue)

Nafasi    : 190

Location: Dar es Salaam
Deadline : Feb 1 2014
Descriptions
Kamishina wa Jeshi la Zima moto na uokoaji anawatangazia Watanzania wenye Sifa kutuma maombi ya kazi kujaza nafasi za kazi zifuatazo :-

Qualifications
Sifa za Mwombaji.
Mwombaji awe amehitimu na kupata cheti cha mtihani wa kidato cha sita.
Mwenye ujuzi katika fani zifuatazo atafikiriwa zaidi.
Na diploma ya kawaida ya Uuguzi au awe na cheti cha majaribio ya ufundi Daraja la 1 katika moja ya fani ya Umakenika , ufundi bomba, ufundi umeme, uchomeaji, ufundi uashi na ufundi seremala.
Kazi za Kufanya
  • Kusimamia kazi za chumba cha mawasiliano;
  • Kusimamia kazi za uzimaji moto na uokoaji;
  • Kuandaa utaratibu wa ukaguzi wa vituo vya maji vya Zimamoto (Fire Hydrants Inspection);Kutunza kumbukumbu za kituo na
  • Kutekeleza kazi nyingine atakazopangiwa na viongozi wake wa kazi.

data-override-format="true" data-page-url = "http://tzjobposition.blogspot.com">

How to apply: 
MASHARTI MUHIMU YA KUZINGATIA.
  • Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 30, mwenye afya njema na ambaye hajaoa au kuolewa.
  • Mwombaji awe hajatenda kosa lolote la jinai.
  • awe tayari kuhudhuria mafunzo ya kijeshi kwa muda usiopungua miezi 6 kabla ya kuajiriwa.
  • Mwombaji awe tayari kufanya kazi mahali popote atakaopopangiwa ndani ya Nchi.
  • Mwombaji aliyehudhuria na kufaulu mafunzo ya Zimamoto na Uokoaji yanayotolewa na Chuo cha Zimamoto na Uokoaji au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali , atafikiriwa kwanza.
  • Waombaji wenye sifa waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa.
  • Barua zote za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya masomo ya kidato cha nne na sita pamoja na vya taaluma/ujuzi, wasifu wa mwombaji(CV),Ikiwa na majina ya wadhamini watatu na anwani zao, nakala ya cheti cha kuzaliwa na picha mbili ndogo za pasipoti.
  •   Mwombaji aandike kazi aliyoomba juu ya bahasha.
  • Mwisho wa kupokea maombi ni Tarehe 1 Februari, 2014.
  • Barua zote za maombi zitumwe kwa njia ya Posta.
  • Mwombaji wa kazi ya Sajini na Konstebo wa Zimamoto na Uokoaji watume barua za maombi kwa anuani ifuatayo;
Kamishina Jenerali,
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
S.L.P 5821,
DAR ES SALAAM.
  • Waombaji wa kazi ya Mkaguzi Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji watume barua za maombi kwa anuani ifuatayo:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
SL.P 9223,
DAR ES SALAAM.

0 Comments: