Home »
» WATANZANIA WAASWA KUEPUKA UGONJWA WA KISUKARI
Imeelezwa kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wanaugua ugonjwa wa
kisukari hali ambayo huchangia na unywaji wa pombe huvutaji wa sigara,
ulaji wa vyakula usiofaa na kutokufanya mazoezi ya mwili. Hayo yamesemwa
leo na Dk. Omary Ubuguyu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH)
wakati akitoa semina kwa waandishi wea habari kuhusu ugonjwa huo leo
jijini Dares Salaam. Aliongeza kuwa asilimia ya idadi ya watu 80 hadi
90 wanaugua ugonjwa huo duniani. “ Unywaji wa pombe kuanzia chupa tano
kwa wanaume na chupa 4 kwa wanawake huchangia kusababisha ugonjwa huu,”
alisema Dk. Ubuguyu.
Kwa upande wake Mratibu wa semina hiyo ,kutoka Mradi wa Taifa wa
Kisukari, John Gardner alisema gharama ya matibabu ya ugonjwa huo
ugharimu dola za Marekani milioni 378 ya asilimia 12 ya bajeti ya afya
duniani kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2010, ambapo inaweza kufikia
hadi zaidi dola milioni 400.
data-override-format="true"
data-page-url = "http://tzjobposition.blogspot.com">
|
 |
Akizungumzia kuhusu ugonjwa huo, Dk. Zakharia Ngoma alisema ulaji
usiofaa na mtindo wa maisha huchangia kwa kiasi kikubwa . Hivyo utumiaji wa vya kula vya asili ,vya kuchemsha, mafuta, chumvi na
sukari kidogo , mboga za majani kwa wingi na matunda kila siku ,
pamoja na vyakula vyenye virutubisho vyote husaidia kuepukana na ugonjwa
huu, ” alisema Dk. Ngoma. Aliongeza kuwa hutumiaji wa vyakula vya jamii
ya kunde na visivyokobolewa husaidia kuepuka ugonjwa huu, ikiwemo
kunywa maji kwa wingi na kuepuka msongo wa mawazo.
0 Comments:
Post a Comment