NAFASI ZA KAZI -AFISAMTENDAJI KIJIJI MISUNGWI -48

HALMASHAURI YA WILAYA YA MISUNGWI


MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MISUNGWI ANAWATANGAZIA WANANCHI NAFASI ZA KAZI MBALIMBALI KAMA IFUATAVYO

1. (A) AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA II (V.E.O II) – TGS C- NAFASI 48

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa kwa waliohitumu kidato cha IV au VI na waliohitimu stashahada au shahada ya juu, Uongozi, Maendeleo ya jamii, kilimo, sheria kutoka vyuo vinavyotambulika na serikali


MASHARTI YA JUMLA
Awe raia wa Tanzania
Awe mwenye maadili mazuri
• Hajafukuzwa kazi
• Hajapunguzwa kazi
• Hajafungwa na kupatikana na kosa la jinai
• Awe tayari kufanya kazi eneo lolote Misungwi bila kuhama kwa kipindi cha miaka 5
• Barua ya maombi iambatanishwe na picha (2) za sasa passport size na vivuli (photocopy) vya vyeti vya elimu na Taaluma
• Andika namba ya simu ya mkononi katika barua ya maombi ili kurahisisha mawasiliano
Mwisho wa kupokea maombi ni 30/05/2015 saa 9:00 alasiri
 
APPLICATION INSTRUCTIONS:

JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yatumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa anuani ifuatayo
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
S.L.P 20
MISUNGWI