Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega amepokea kibali
chaajira mpya kwa barua ya tarehe 7 Desemba 2017 yenye Kumbu Na. FA.
170/533/01/38 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Raisi Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa hiyo anawatangazia wananchi wote
wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 14 za kazi kwa kada mbali mbali
kama zilivyoorodheshwa hapo chini
KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III NAFASI 2 TGS B
SIFA ZA MUOMBAJI;
Wenye elimu ya kidato cha nne (IV), waliomaliza mafunzo ya uhazili
na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya
Kiswahili na Kiingereza maneno 80kwa dakika moja na wawe wamepata
mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na
kupata cheti katika Programu za Windows, Microsoft Office, Internet,
E-mail na Publisher.
KAZI MAJUKUMU YA KUFANVA
i. Kuchapa barua, taarifa na nyarakaza kawaida
ii. Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanayoweza kushughulikiwa.
iii. Kusaidia kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, wageni,
tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine
zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu
Mkuu wake kwa wakati unaohitaji
iv. Kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada, nyaraka au
kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
v. Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake w akazi kwa wasidizi
wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na
wasaidizi hao.
vi. Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa waliokatika
sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu
zinazohusika.
vii. Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi
=============
MTENDAJI WA KIJIJI III NAFASI 7 TGS B
sifa za jumla
- mwenye elimu ya kidao cha IV au VI aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo Utawala , Sheria, Elimu
ya jamii usimamizi wa fedha maendeleo ya jamii na sayansi ya jamii
kutoka chuo cha Serikali za mitaa Homboro Dodoma au chochote kinacho
tamblika na serikali
KAZI NA MAJUKUMU
- afisa masuuli na mtendaji mkuu wa Serikali ya Kijiji
- atawajibika kwa mtendaji wa kata
- kuandaa taaarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na
kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoo
njaa, umaskini na na kuongeza uzalishaji mali
- kukusanya mapato ya Halmashauri ya Wilaya
- kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji
- kutafsiri na kusimamia era, sheria na taratibu
- kupokea kusikiliza na kutatua mogogoro ya wanancgi
- atawajibika kwa mtendaji kata
- kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao
- kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipnago ya maendeleo ya kijiji
- katibu wa mikutano ya kamatai zote za Halmashauri ya KIJIJI
- KIiongozi mkuu wa vitengo vya kitaalam katika kijiji
- mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji nk
============
DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 5 TGS B
SIFA ZA KUINGILIA
Kuajiriwa mwenye cheti cha mtihani wa kidato cha 4 au 6 wenye
leseni ya daraja c ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari
kwa muda usiopungua miaka mitatu bila ksababisha ajali
KAZI ZA KUFANYA
- kuendesha magari ya abiria namaroli
- Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri na usafi
wakati wote na kufanya Uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili
kugundua ubovu unaohitaji matengenezo.
- Kufanya matengenezo madogomadogo katika gari.
- Kutunza na kuandika daftari la Safari “Log – book” kwa Safari zote.
- kufanya matengenezo madogo madogo katika gari
=============
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II – NAFASI 2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha IV au VI wenye cheti cha
utunzaji kumbukumbu kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na serikali
KAZI NA MAJUKUMU
Wasaidizi wa kumbukumbu watafanya kazi zifuatazo hapa chini kwa
kuzingatia fani walizosomea na kazi wanazofanya ni kama vile uhifadhi wa
nyaraka, uhifadhi wa kumbukumbu za afya, ardhi na masjala ya kawaida
KAZI ZA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II
i. Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomi
ii. Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka
iii. Kuchambua , kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka
katika makundi kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa
ajili ya matumizi ya ofisi
iv. Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu
v. Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka n.k) katika mafaili
vi. Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali
MAHSRTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE
i. mwombaji awe raia wa Tanzania na awena umri usiozidi miaka 45
ii. waombaji waambatanishe nakala za vyeti vya kuzaliwa
iii. maombi yaaambatane na vyeti vya taaluma vyeti ya elimu ,
cheti cha kuzaliwa, na picha 2 passport za rangi za hivi karibuni na
iandikwe jina nyuma
iv. picha moja ya passport size ya hvi karibuni
v. hati za matokeo hazitakubaliwa
vi. waombaji aambao ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia katika
utumishi wa umma wasiomba na wanapaswa kuzingatia katika maelezo
yalioko katika waraka Na. cac.45/257/01/d/140 WA TEREHE 30, NOVEMBA
2010
vii. maombi yaandikwe kwa lugha ya kiswahili au kingereza na
yatumwe kwa njia ya posta kabla ya tarehe 01/01/2018 kwa anuani
ifuatayo
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA ,
S.L.P 157,
BUSEGA.
0 Comments:
Post a Comment