NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KARATU

KUMBU NO. KDC/DED/CS 1/17/VOLIII/63
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa za kuomba nafasi za ajira ya kudumu kwa nafasi za Mtendaji wa Kijiji daraja la III kwa kusingatia maelezo ya kazi zilizoainishwa hapo chini

 

MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 11
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu elimu ya kidato cha Sita/Nne na Mafunzo ya Astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma, au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI ZA KUFANYA
– Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
– Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao.
– Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
– Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
– Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
– Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na Kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
– Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.
– kukusanya mapato ya Halmashauri ya Wilaya
– kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji
– kutafsiri na kusimamia era, sheria na taratibu
– kupokea kusikiliza na kutatua mogogoro ya wanancgi
– atawajibika kwa mtendaji kata
– kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao
– kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipnago ya maendeleo ya kijiji
– katibu wa mikutano ya kamatai zote za Halmashauri ya KIJIJI
– KIiongozi mkuu wa vitengo vya kitaalam katika kijiji
– mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji nk
– atawajibika kwa mtendaji wa kata
MASHARTI YA AJIRA – Ajira ya kudumu
NGAZI YA MSHAHARA
cheo cha Afisa Mtendaji wa Kijiji iii kina mshahara wa TGS B1 sawa na Tshs 390,000/= hadi 489,000/= kwa mwezi
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
– waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 mpaka 45
– waombaji lazima waambatanishe wasifu wao wenye mawasiliano ya uhakika anwani , barua pepe, na namba za simu
– waombaji waombe kwa kuzingatia masharti ya tangazo la kazi
– waombaji wote lazima wawe na nakala za vyeti vifuatavyo
– ASTASHAHADA/CHETI CHA TAALUMA KULINGANA NA SIFA HUSIKA
– cheti cha kuhitimu mtihani wa kidato cha 4 au 6
– cheti cha kuzaliwa
– hati ya matokeo ya kidato cha 4 haitakubaliwa
– kuwasilisha statement of results/transcripts bila cheti haitakubaliwa
– kuwasilisha cheti cha kughushi na maelezo mengine itasababisha kuchukuliwa hatua za kisheria
– waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba nafasi hii
– waombaji mabao walistaafu kazi kwasababu yoyote ile hawaruhusiwi kuomba nafsi hii
– waombaji waonyeshe wadhamini wawili na mawasiliano yao anwani na namba zao za simu
– waombaji wenye cheti cha nje wahakikishe vimehakikiwa na NACTE au NECTA
– Barua ya maombi iandike kwa kiswahili au kingereza
– watakaochaguliwa kwenye usaili watajulishwa
– waombaji wote wanatakiwa wawe na cheti cha NTA Level 5 na kuendelea
– mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 21 February 2018
maombi yatumwe kwa
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA KARATU ,
S.L.P 190,
KARATU

0 Comments: