MHASIBU MSAIDIZI – OSHA

Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi ni Taasisi ya Serikali ilioundwa kwa mujibu wa Sheria ya Wkala wa Serikali namba 30 ya mwaka 1997 ambapo majukumu yake yameainishwa katika heria ya usalama na afya mahala pa kazi namba 5 ya mwaka 2003. Wakala pamoja na kazi nyingine una dhamana ya kusimamia usalama na afya za wafanayakazi wanapokuwa kazini, ilikuhakikisha kuwa wakala unatekeleza majukumu kama yalivyoainishwa katika sharia tajwa hapo juu, Mtendaji Mkuu anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi zifuatazo

MHASIBU MSAIDIZI NAFASI 4 (MARUDIO)

SIFA ZA WAOMBAJI
- Awe na stashahada ya kawaida ya uhasibu kutoka chuo / taasisi yoyote inayotambuliwa na serikali
- Awe na cheti cha ufahulu wa mtihan mgumu wa uhasibu serikalin unaotolewa na chuo Cha Utumishi wa Umma
- Awe na uzoefu wa kazi usiopungua mwaka mmoja katika fani ya uhasibu

MAJUKUMU YA KAZI
i. Kupoka na kulipa fedha
ii. Kutunza daftari la fedha
iii. Kufanya usukuhisho wa hesabu za benki (bank reconciliation)
iv. Kukagua hati za malipo
v. Kupitisha malipo kulingana na kanuni za fedha
vi. Kusimamia kazi za wasaidizi wa hesabu
vii. Kufanya kazi nyingine atakayopangiwa na msimamizi wake

MSHAHARA
OSHA 4.1

MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe raia wa Tanzania na wenye umri usiozid miaka 45
- Waombaji waambatanishe vyeti vya kuzaliwa
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza yeneye anuani na namba za simu pamoja na majina ya wadhamini wa 3
- Maombi yaambatanae na vyeti vya taaluma maelezo na nakala za vyeti vya kidato cha 6 kwa wale waliofika kiwango hicho na cheti cha kuhitimu mafunzo mbali mbali kwa kuzingatia kazi husika
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika TCU/NACTE
- Watakao wasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria
- Maombi yatumwe kwa njia yay a posta au kwa mkono kufikisha ofisi za makao makuu zilizopo kinondoni barabara ya mahakama
- Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 06/02/2018
- Maombi yatakayowasilisha nje ya utaratibu uloanishwa hayatafanyiwa kazi

Jinsi ya kuwasilisha maombi
Maombi yatumwe kwa

MTENDAJI MKUU,
WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI,
S.L.P 519,
DAR ES SALAAM
Source Mwananchi January 25, 2018

Related Posts:

0 Comments: