MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III - NAFASI 9

Awe amehitimu elimu ya kidato cha Sita/Nne na Mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma, au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI ZA KUFANYA
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
- Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao.
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
- Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
- Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na Kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.

2.3. MSHAHARA
TGS B1 - Tshs 390, 000/= hadi Tshs 489,000/=


MAMBO YA KUZINGATIA
- mwombaji awe raia wa Tanzania
- awe na umri kati ya miaka 18 hadi 45
- barua zote ziandikwe kwa mkono na ziambatanishwe na nyaraka zifuatazo
- maelezo binafsi
- nakala za vyeti vya kidato cha 4 au 6 cheti cha kuzaliwa na vyeti vya elimu ya taluma
- picha ndogo 2 passport size za hivi karibuni

transcript, testimonial results havitakubaliwa
- mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 09/03/2018
- maombi yatakayoletwa baada ya muda ulowekwa katika tangazo hayatopokelewa
- tangazo hili linapatikana kwenye tovuti ya Halmashauri www.kilolodc.go.tz

Barua zitumwe kwa

MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOLO,
S.L.P 2324,
KILOLO.

Mwisho wa kutuma maombi  9 March 2018

0 Comments: